Tuesday, April 16, 2013

WAZIRI WA FEDHA ZIMBABWE ASEMA NCHI HAINA PESA KWA AJILI YA UCHAGUZI


Waziri wa Fedha wa Zimbabwe amesema kuwa, nchi hiyo haina uwezo wa kudhamini gharama za kuendesha zoezi la uchaguzi rais nchini humo. Tendai Biti ameliambia Bunge la Zimbabwe kuwa, hazina iliyopo ya serikali haiwezi kudhamini gharama za kuitisha uchaguzi nchini humo. Biti ameongeza kuwa, Harare inahitajia kiasi cha dola milioni 132 ili kuitisha uchaguzi wa rais.
Hayo yanaelezwa katika hali ambayo, chama cha Zanu PF kinachoongozwa na Rais Robert Mugabe kinasisitiza juu ya kufanyika uchaguzi wa rais mwezi Juni mwaka 2013 badala ya mwishoni mwa mwaka huu.
Waziri wa Fedha wa Zimbabwe amesema kuwa, serikali ya Harare licha ya kuandika barua ya kuomba msaada kutoka Umoja wa Mataifa, imeandika barua nyingine kwa serikali za Afrika Kusini na Angola ili kuomba msaada wa kuitisha uchaguzi huo wa rais.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO