Thursday, April 11, 2013

UN YAIKOSOA ISRAEL KWA VIZUIZI VYAKE HUKO GHAZA

Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa James W Rawley amesema kuwa, vikwazo vipya vya Israel kwa watu wa Ukanda wa Gaza unaozingirwa vimesababisha uhaba mkubwa wa chakula kwenye eneo hilo. Rawley ameongeza kuwa, Israel imetangaza vizuizi kadhaa vya kuingia watu na bidhaa kwenye Ukanda wa Gaza, ikiwa ni pamoja na kufunga kivuko cha Kerem Shalom. Mratibu huyo wa Misaada wa Umoja wa Mataifa amesema, hatua hiyo imesababisha kupungua mahitaji muhimu ya chakula, nishati ya kupikia pamoja na kukiukwa haki muhimu za wananchi wa Gaza na kwamba iwapo vizuizi hivyo vitaendelea, wananchi wa Gaza watakabiliwa na matatizo makubwa.
Inafaa kuashiria kuwa, kivuko cha Kerem Shalom kilichofungwa na utawala wa Kizayuni ni kivuko pekee kinachounganisha Ukanda wa Gaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Tangu mwaka 2007 eneo hilo liko chini ya mzingiro mkali wa Israel, unaofanya maisha ya wakaazi wa eneo hilo yawe magumu sana.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO