Muungano wa upinzani nchini Syria umeitaka serikali ya Lebanon idhibiti mipaka yake baada ya waasi kusema wemelishambulia eneo la mpakani kujibu mashambulio yaliyofanywa na kundi la Hezbollah. Muungano huo pia umeitaka Lebanon ikomeshe mara moja harakati za kijeshi za kundi hilo la Kishia katika ardhi ya Syria. Kwa wiki kadhaa sasa makundi yenye mafungano na Hezbollah yamevishambulia vijiji ndani ya Syria kwenye mpaka kati ya Syria na Lebanon. Kauli hiyo ya muungano wa Syria inakuja baada ya Lebanon kusema itawasilisha waraka kulaani kuenea kwa mashambulio katika ardhi yake kutoka Syria. Waasi wa Syria wanadai walifyatua makombora nchini Lebanon mwishoni mwa wiki iliyopita, wakiwalaumu wapiganaji wa kundi la Hezbollah kwa kuzishambulia kutokea Lebanon ngome za waasi katika eneo lililokumbwa na mzozo la Qusayr karibu na mpakani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO