Tuesday, April 16, 2013

WANAJESHI WA UN KUWASILI MALI JULAI


Wanajeshi 11,000 wanatarajiwa kuchukua Oparesheni ya kijeshi nchini Mali kutoka kwa Ufaransa kuanzia tarehe 1 mwezi wa Julai mwaka huu ikiwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litapisha azimio la kuwaruhusu kwenda nchini humo. Baadaye mwezi huu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litapitisha azimio lingine la kuruhusu jeshi la Ufaransa kuingilia Oparesheni hiyo ikiwa wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa watakaokuwa na kibarua cha kulinda amani watavamiwa na waasi wa Kiislamu.

Wanajeshi wa Ufaransa waliingia Mali mwezi Januari mwaka huu kukabiliana na waasi wa Kislamu Kaskazini mwa nchi hiyo na tayari wanajeshi hao wameaza kuondoka nchini humo lakini serikali ya Paris imesema kuwa itawaacha wanajeshi elfu moja kusaidiana na wale wa Umoja wa Mataifa.  Wanajeshi zaidi ya 8,000 kutoka barani Afrika wako nchini Mali lakini wanajeshi wa Chad wameanza kuondoka nchini humo kuweka mikakati ya kupisha jeshi la Umoja wa Mataifa ambalo litakuwa na jukumu la kuhimiza amani kwa kipindi cha miezi kumi na miwili.

Baraza la Usalama la Umoaj wa Mataifa linakutana siku ya Jumatano kujadili hali ya usalama nchini humo na Oparesheni hiyo ya kulinda amani. Serikali ya Mali imesema kuwa uchaguzi wa urais na wabunge utafanyika mwisho wa mwezi wa Julai.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO