Takriban watu 28 wameuawa katika shambulio la bomu na risasi
mjini Mogadishu Somalia. Wengine hamsini wakiwemo washambuluaji tisa pia wanasemekana kuuawa baada ya
mtu aliyekuwa amejihami kuvamia majengo ya mahakama na kuanza kushambulia watu
kiholela. Baadaye bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari lilipuka kando ya barabara
inayoelekea katika uwanja wa ndege ambako wafanyakazi wawili wa misaada wa
Uturuki walikuwepo
Kundi la wapiganaji la al-Shabab linasema ndilo limefanya shambulio hilo. Al-Shabaab, ambalo lina uhusiano na al-Qaeda, limelaumiwa kwa mashambulio
kadhaa mjini Mogadishu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Lakini wadadisi wanasema kuwa mashambulizi yaliyotokea hapo jana ndio mabaya
zaidi kushuhudiwa tangu wapiganaji wa Al Shabaab kufukuzwa Mogadishu mwaka
2011. Sasa shambulio hilo limesababisha hali ya hofu miongioni mwa wakaazi wa
Mogadishu.
Sio eti ni mashambulizi makubwa kuwahi kushuhudiwa Mogadishu , bali yametokea
huku wakaazi wa Mogadishu ukianza kuwa mji wenye utulivu. Mashambulizi hayo bila shaka yatakuwa changamoto kubwa kwa serikali katika
mji mkuu. Polisi wamepelekwa katika miji mikubwa ili kutoa ulinzi kwa majengo ya
serikali. Lakini serikali katika siku za nyuma ilikubali kuwa inaweza tu kufanya kadri
ya uwezo wake kujaribu kuzuia washambuliaji wa kujitoa mhanga. Vifo vya wafanyakazi wa misaada kutoka Uturuki, pia vitazua wasiwasi miongoni
mwa idadi inayoongozeka ya mashirika ya misaada inayofanya kazi Somalia
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO