Harakati ya Ukombozi ya Niger Delta (MEND) imetishia kuanzisha tena
mashambulizi yake dhidi ya Misikiti, taasisi za Kiislamu na kuwauwa viongozi wa
Kiislamu. Harakati ya Ukombozi ya Niger Delta jana usiku ilitoao taarifa na
kuwatishia Waislamu wa Nigeria kuwa itaishambulia misikiti, taasisi za Kiislamu,
mikusanyko ya waumini wa Kiislamu katika maeneo matukufu na kuwauwa viongozi wa
Kiislamu. Taraifa hiyo imeongeza kuwa mashambulizi dhidi ya misikit na vituo vya
Kiislamu yataanza tarehe 30 mwezi ujao. Harakati ya Ukombozi ya Niger Delta huko
nyuma ilitishia kuanzisha tena mashambulizi yake kama radiamali kwa hukumu ya
kifungo cha miaka 24 jela iliyotolewa kwa Henry Okah kiongozi wa zamani wa kundi
hilo na mahakama moja ya Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO