Monday, May 13, 2013

19 WAJERUHIWA SHAMBULIO LA SILAHA MAREKANI

Watu 19 wamejeruhiwa baada ya watu waliokuwa na silaha kuwafyatulia risasi katika jimbo la Louisiana nchini Marekani. Polisi ya Marekani imetangaza kuwa, tukio hilo lilijiri katika sherehe za Siku ya Mama zilizofanyika katika mji wa New Orleans uliopo katika jimbo la Louisiana. Watoto wawili wa miaka 10 ni miongoni mwa majeruhi wa shambulio hilo. Aidha polisi imetangaza kuwa, shambulizi hilo limefanywa na watu watatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 kila mmoja. Hata hivyo baada ya washambuliaji hao kutekeleza hujuma hiyo walifanikiwa kukimbia eneo la tukio bila kutiwa mbaroni. Hii ni katika hali ambayo siku ya Jumapili pia polisi ilionyesha miili ya watu wanne waliouawa kwa kupigwa risasi ndani ya nyumba moja katika jimbo la Indiana Kusini mwa nchi hiyo. Itakumbukwa kuwa mnamo mwezi Disemba mwaka jana kulitokea mauaji makubwa dhidi ya wanafunzi wa shule ya msingi katika mji wa New Town katika jimbo la Connecticut, mauaji ambayo yaliwatia wasiwasi mkubwa wananchi wengi wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO