Kumeshuhudiwa mapigano mapya kwa siku ya tatu mfululizo mashariki mwa mji wa Goma nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji waasi wa kundi la M23 wakati huu katibu mkuu wa umoja wa mataifa UN Ban Ki Moon akitarajiwa kuzuru mjini Goma. Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo lilitangaza kwamba lipo tayari kusitisha mara moja mapigano dhidi ya vikosi vya serikali ya Congo FARDC ili kutoa nafasi ya ziara ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon katika jiji la Goma.
Katika taarifa iliyotolewa na kundi hilo kupitia Amani Kabasha anayehusika na mawasiliano katika kundi hilo, imesema M23 inaarifu jumuiya ya kimataifa kwamba ipo tayari kusitisha vita, wakati huu Ban Ki Moon akizuru jiji la Goma mashariki mwa DR Congo Alhamisi hii wakati mapigano baina ya waasi hao na wanajeshi wa serikali yakishuhudiwa. Mapigano hayo yamefanya mkuu wa tume ya usalama kwenye Umoja wa Afrika AU, Ramtan Lamamra kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya wapiganaji wa M23 na kuongeza kuwa makundi ya uasi yasiruhusiwe kupoteza amani. kwa upande wa wabunge wa Upinzani wao wanaona kuwa kutopewa nafasi ya kuwa na mzungumzo ya faragha na katibu mkuu Ban hakuna maana kwenye ziara yake na kwamba amekuja kutalii na upinzani haukubaliani nae.
Kwenye mazungumzo yake na rais Joseph Kabila wa kabange na waziri mkuu Matata Mponyo katibu mkuu Ban amesema vikosi vilivyoidhinishwa na umoja huo vitafanya kazi kwa kuzingatia haki za binadamu katika kuwashughulikia waasi hao. Wabunge wa upande wa chama tawala cha PPRD wanasema ziara hiyo inaleta matumaini mapya kwa wananchi wa mashariki mwa Congo kwakua jumuiya ya kimataifa iko pamoja nao. Tayari Vikosi vya Tanzania, malawi na Afrika kusini vinatarajiwa kuanza operesheni maalumu ya kukabiliana na waasi wa M23 punde baada ya kuwasili kwa wanajeshi wote.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO