Maafisa wa Iran wamezuwia wagombea wawili maarufu kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao wa urais, na kuhakikisha kuwa wanaogombea ni miongoni mwa wale watiifu kwa kiongozi wa kidini nchini humo. Baraza la uangalizi lilimuondoa katika orodha ya wagombea rais wa zamani Akbar Hashemi Rafsanjani na Esfandiar Rahim Mashaei, msaidizi mkuu wa rais wa sasa Mahmoud Ahmedinejad. Rafsanjani amesema hatapinga uamuzi huo katika azma yake ya kugombea tena urais.
Esfandiar Rahim Mashaie , msaidizi wa karibu wa rais anayeondoka madarakani Ahmedinejad, pia ameondolewa katika orodha ya wagombea katika uchaguzi huo. Watu hao wawili wamekuwa mara kwa mara wakipingana na kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei. Wengi wa wagombea wanane katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika duru ya kwanza Juni 14 ni watiifu kwa Khamenei.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO