Marekani na Israel zimeongeza matumaini ya kuanza tena kwa hatua za kuleta amani katika mashariki ya kati , licha ya kutokuwepo dalili muhimu hadi sasa katika juhudi za miezi miwili za waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry kuzileta pande mbili za Waisrael na Wapalestina katika meza ya mazungumzo.
Akifanya ziara yake ya nne nchini Israel tangu kuchukua wadhifa huo Februari mwaka huu, Kerry alimsifu waziri mkuu Benjamin Netanyahu kwa jinsi anavyotafuta kwa dhati njia za kurejesha matumaini ya amani. Kerry ameonyesha matumaini bila ya kuainisha mikakati maalum ya kumaliza mkwamo kati ya pande hizo mbili ambazo hazijafanya majadiliano ya ana kwa ana katika muda wa miaka minne na nusu iliyopita. Kerry anatarajiwa kukutana na rais wa mamlaka ya Palestina mjini Ramallah leo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO