Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague amesema leo kuwa Iran na kundi la wanamgambo wa Hezboullah wameongeza msaada wao wa kijeshi kwa utawala wa rais Bashar al-Assad wa Syria. Hague ameuambia mkutano na waandishi habari kuwa utawala wa Syria unapata msaada mkubwa katika miezi ya hivi karibuni kutoka nje ya nchi hiyo. Shutuma zake zinaakisi madai kutoka kwa upinzani nchini Syria kuwa wapiganaji kutoka Iran na Hezboullah wanaunga mkono majeshi tiifu kwa al-Assad.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema kuwa jumuiya ya kimataifa itaongeza msaada wake kwa upinzani iwapo rais Bashar al-Assad hatakubali kushiriki katika mazungumzo na upinzani. John Kerry ameyasema hayo katika mkutano na waandishi habari leo baada ya mkutano wa mataifa 10 yanayounga mkono upinzani nchini Syria akisisitiza kuwa mkutano huo ni juhudi za kumaliza mauaji nchini humo.
Wakati huo huo balozi wa Syria nchini Jordan ameshutumu mkutano wa mataifa ambayo yanaunga mkono upinzani nchini Syria , na kuuita mkutano huo kuwa ni sehemu ya kampeni ya Marekani na Israel kuiharibu nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO