Kundi kuu la upinzani nchini Syria la muungano wa kitaifa limeanza mkutano wao mjini Istanbul leo. Wapinzani wanajadili pendekezo la Urusi na Marekani kuwaleta pamoja waasi na maafisa wa serikali ya rais Bashar al-Assad katika meza ya majadiliano. Katika mkutano wao wa siku tatu , muungano huo pia unatarajiwa kumchagua rais mpya, watajadili kuhusu upanuzi na kujumuisha wajumbe wapya katika baraza la taifa na kuamua hatma ya serikali ya mpito ya waasi. Mkutano huo unakuja wakati waasi wanakabiliwa na mashambulio makubwa ya majeshi ya rais Bashar al-Assad na kundi la wanamgambo wa Hezboullah katika mji wa Qusayr ambao ni ngome ya waasi katikati ya Syria. Mjumbe wa muungano huo Salem al-Moslet amesema kandoni mwa mkutano huo kuwa sharti muhimu ni kuwa rais Assad ajiuzulu, chini ya juhudi hizo za amani za Urusi na Marekani zinazojulikana kama Geneva mbili.
Wakati huo huo maafisa wa usalama nchini Lebanon wamesema watu watano wameuwawa katika mapigano usiku wa jana kati ya wapinzani na waungaji mkono wa utawala wa Syria nchini Lebanon katika mji wa Tripoli.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO