Syria imesema kwamba shambulizi la hivi karibuni la Israel dhidi ya nchi hiyo ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa na kwamba shambulio hilo linafungua mlango wa kila jambo.
Waziri wa Habari wa Syria Omran al Zuhbi amesema hayo baada ya kikao cha dharura cha serikali ya Damascus hapo jana na kuongeza kuwa, Syria ina haki na wajibu wa kulinda watu wake kwa kila njia bila kuogopa mashambulizi ya Israel.
Ameongeza kuwa, shambulio la Israel nchini Syria limelifanya eneo la Mashariki ya Kati kuwa hatari zaidi na kwamba serikali bado inaangalia namna ya kujibu shambulio hilo. Waziri wa Habari wa Syria ameongoza kwamba, huo ni ushahidi wa wazi kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel unashirikiana na waasi wa Syaria wanaopigana dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Assad.
Kabla ya hapo pia Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria ilituma barua tofauti kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama na kuelezea kwamba mashambulizi ya Israel nchini humo yanaonyesha jinsi Tel Aviv inavyoshirikiana na makundi ya kigaidi ya Syria yakiwemo ya ala Qaida na al Nusra.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO