Wednesday, May 22, 2013

MUGABE ATIA SAINI YA KATIBA MPYA

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe leo ametia saini katiba mpya ya nchi hiyo. Taarifa kutoka Harare zinasema kuwa, tukio la kutiwa saini katiba mpya ya nchi hiyo linafuatia zoezi la kura ya maoni lililofanyika mwezi Machi mwaka huu nchini Zimbabwe, na kwamba kwa mujibu wa katiba hiyo mpya, madaraka ya rais yatapunguzwa na hali kadhalika kipindi cha urais hakitazidi mihula miwili ya miaka mitano mitano. Eric Matinenga Waziri wa Katiba wa Zimbabwe amesema kuwa, 'leo ni siku ya kihistoria, siku inayoainisha mustakbali wa nchi'. Matinenga amesema kuwa, Rais Mugabe ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 89 anaweza kushiriki kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi ujao wa rais. Imeelezwa kuwa, uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika mwaka huu, unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa dola milioni 130 za kuendeshea uchaguzi huo. Hadi sasa haijawekwa wazi kama wasimamizi kutoka mataifa ya kigeni wataruhusiwa kuwa waangalizi katika uchaguzi huo au la.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO