Katibu Mkuu wa chama cha Kiislamu cha 'Umma' nchini Saudi Arabia amesema kuwa, zaidi ya watu elfu 30 wanashikiliwa kwenye jela za utawala wa kifalme wa Aal Saud nchini humo. Muhammad bin Saad Aal Mufarrah amesema kuwa, wafungwa hao wa kisiasa wanahitajia uungaji mkono wa wananchi ili waweze kutolewa kwenye jela za utawala wa Aal Saud. Katibu Mkuu wa chama cha Umma amesema kuwa, wengi kati ya mahabusu hao wanaoshikiliwa kwenye jela za Saudi Arabia hawajafunguliwa mashtaka na wengine hawajui wanatuhumiwa kwa makosa gani. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kwa miezi kadhaa sasa wananchi wa Saudi Arabia katika miji mbalimbali wamekuwa wakifanya maandamano ya amani yenye shabaha ya kuushinikiza utawala wa kifalme wa Saudi Arabia ufanye mabadiliko ya kimsingi, ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo ya wananchi wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO