Washambuliaji wawili wakiwa na visu na panga wamemuua mtu anayeaminika kuwa ni mwanajeshi katika mtaa mmoja kusini mashariki ya London. Polisi inaliangalia tukio hilo la mauaji kuwa ni shambulio la kigaidi. Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amefupisha ziara yake nchini Ufaransa na kurejea haraka mjini London kwa ajili ya mkutano wa dharura wa usalama wa taifa.
Watu hao wawili walimkata mtu huyo kwa visu na panga mbele ya watu waliokuwa wakipita mtaani na walibaki katika eneo hilo wakipaaza sauti zao huku wakipunga silaha zao zilizotapakaa damu. Baadhi ya vyombo vya habari vimesema kuwa watu hao walipaza sauti wakisema maneno kwa lugha ya Kiarabu. Polisi wamesema maafisa waliofika katika tukio hilo waliwapiga risasi na kuwajeruhi watuhumiwa hao. Wote wamepelekwa hospitalini, mmoja akiwa katika hali mbaya.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO