Gazeti la Haaretz linalochapishwa huko Israel limewanukuu viongozi na wanadiplomasia wa utawala wa Israel wakisema kuwa, Uingereza imeongeza mashinikizo yake dhidi ya nchi za Italia, Ufaransa, Ujerumani na Uhispania ili ziitumbukize harakati ya Hizbullah ya Lebanon kwenye orodha ya makundi ya kigaidi. Gazeti la Haaretz limeandika kuwa, licha ya mashinikizo hayo lakini nchi hizo za Ulaya zimekataa takwa la Uingereza, kwa vile hakuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha kuwa Hizbullah inatekeleza operesheni za kigaidi. Mkakati wa kuiweka Hizbullah kwenye kundi la kigaidi, ulipamba moto mwaka jana baada ya kutokea mlipuko nchini Bulgaria na kusababisha watalii kadhaa wa Kizayuni kuuawa na kujeruhiwa. Baada ya kujiri mlipuko huo, utawala wa Kizayuni wa Israel uliituhumu Hizbullah kuwa ndiyo iliyotekeleza shambulio hilo, tuhuma ambazo mpaka leo bado hazijathibitishwa na vyombo vya usalama nchini Bulgaria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO