Saturday, June 08, 2013

ETHIOPIA YATAKA MISRI KUTOA JUU YA UJENZI WA BWAWA

Ethiopia imemuita balozi wa Misri mjini Addis Ababa na kutaka maelezo kuhusiana na matamshi inayodai kuwa ya kiadui yaliyotolewa na wanasiasa wa Misri kuhusu ujenzi wa bwawa la Ethiopia katika Mto Nile. Dina Mufti msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ethiopia amesema, Tarek Ghoneim Balozi wa Misri mjini Addis Ababa ameitwa ili aeleze juu ya matamshi hayo ya kiadui. Mwanzoni mwa wiki hii wanasiasa wa Misri walitahadharisha juu ya kupunguzwa fungu la maji la Misri katika Mto Nile, huku wakipendekeza mpango wa kuhujumu au kuwasaidia waasi dhidi ya serikali ya Addis Ababa ambayo imeanza ujenzi wa bwawa kubwa katika Blue Nile wiki iliyopita ili kuzalisha umeme. Pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mohammed Kamel Amr jana alisema kwamba, usalama wa maji wa nchi yake hauwezi kupuuzwa na kutoa wito wa kutafutwa suluhisho la amani la suala hilo na nchi jirani za Sudan na Ethiopia.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO