Wanaharakati wanaounga mkono Palestina duniani kote wamepanga leo kufanya maandamano ya kutaka kukombolewa Quds Tukufu na maeneo yote ya Palestina. Maandamano hayo ya amani ya kupinga utawala wa Kizayuni wa Israel yaliyopewa jina la ‘Maandamano ya Kimataifa ya al Quds’ yanafanyika leo huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Ukanda wa Gaza, Marekani, Uingereza, Canada, Ujerumani, Uturuki, Yemen, Indonesia na nchi nyingine nyingi duniani. Maandamano hayo ya kimataifa ya al Quds hufanyika kila mwaka katika kukumbuka kukaliwa kwa mabavu eneo la Mashariki mwa Quds na askari wa utawala haramu wa Israel wakati wa Vita vya Siku 6 mwaka 1967.
Maandamano hayo pia yatadhihirisha sauti za walimwengu za kupinga kupanuliwa kusiko halali vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel za Palestina, na pia siasa za kibaguzi za Tel Aviv dhidi ya Wapalestina.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO