Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amemtangaza Hassan Ruhani kuwa mshindi wa duru ya 11 ya uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu. Akizungumza mbele ya waandishi usiku huu Mustafa Muhammad Najjar ametangaza kuwa Hassan Ruhani, amekuwa rais mpya wa Iran baada ya kupata kura 18, 613, 329 sawa na asilimia 50.70 ya kura zote. Waziri wa Mambo ya Ndani ameongeza kuwa jumla ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa 11 wa rais ni 36, 704, 156. Muhammad Najjar amesema asilimia 72.7 ya wananchi waliokuwa wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi wa rais walishiriki katika uchaguzi huo uliofanyika jana na kufanikisha kwa maana halisi “Hamasa ya Kisiasa” nchini. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amefafanua kuwa kuanzia saa za awali za upigaji kura wananchi wa Iran walijitokeza kwa wingi katika vituo vya upigaji kura hapo jana, na kutokana na hatua yao ya kupiga kura walitimiza wajibu wao wa kidini na wa kitaifa na kutoa mchango wao ipasavyo katika kuainisha mustakabali wa nchi yao
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO