Wednesday, June 05, 2013

JESHI LA SYRIA LAUDHIBITI MJI WOTE WA QUSAYR

Televisheni ya taifa ya Syria imeripoti kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuudhibiti kikamilifu mji wa kistratejia wa Qusayr baada ya mapigano makali ya siku kadhaa na makundi ya kigaidi. Habari zinasema kuwa, makumi ya magaidi wameuawa, baadhi yao wamekamatwa au kujisalimisha huku wengine wakikimbia nje kabisa ya mji huo. Wanaofuatilia kwa karibu matukio ya Syria wanasema ushindi huo wa serikali ni pigo kubwa kwa magaidi wanaofadhiliwa na Marekani na waitifaki wake wa Ulaya na Mashariki ya Kati. Mji huo wa Qusayr ulioko karibu na mpaka wa Syria na Lebanon umekuwa chini ya udhibiti wa magaidi kwa muda mrefu lakini mapigano ya wiki kadhaa kati ya makundi hayo na vikosi vya serikali yameonyesha wazi kwamba jeshi la Rais Bashar Asad bado lina nguvu na uwezo wa kuzima ugaidi nchini humo. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa ujumbe wa pongezi kwa serikali, jeshi na wananchi wa Syria kwa ushindi huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO