Mgombea ukansela wa chama cha SPD katika uchaguzi mkuu nchini Ujerumani Peer Eteinbrück , ametoa hotuba mjini Berlin akiainisha mapendekezo yake katika sera za mambo ya kigeni. Ni mgombea mkuu anayepambana na kansela Angela Merkel katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Septemba. Steinbrück ameelezea upinzani wake dhidi ya ununuzi wa ndege za kijeshi zisizo na rubani, baada ya mradi wa kuziendeleza kufutwa na serikali mwezi uliopita. Steinbrück pia ameahidi kupunguza mauzo ya silaha na kusema anapinga hatua ya kutuma silaha kwa waasi nchini Syria. Pia amemshutumu kansela Merkel kwa uongozi unaoelemea upande mmoja katika mzozo wa mataifa ya kanda ya euro. Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura kwa uchaguzi wa hapo Septemba unaonesha chama cha Merkel cha siasa za wastani za mrengo wa kulia CDU na SPD cha Peer Steinbrück cha siasa za wastani za mrengo wa shoto hawiwezi kupata ushindi moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO