Sunday, June 09, 2013

KARZAI ATAKA UINGEREZA IKABIDHI WATU INAOWAKAMATA AFGHANISTAN

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amevipa vikosi vya Uingereza muda ya wiki mbili kuwakabidhi kwa serikali ya Kabul Waafghani wote wanaowashikilia katika kambi ya kijeshi ya Bastion. Tangazo hilo limetolewa na msemaji wa Karzai baada ya kufichuliwa wiki iliyopita kwamba vikosi vya Uingereza nchini Afghanistan vinawashikilia Waafghani 90 bila kufunguliwa mashtaka. Msemaji wa Rais Karzai amesema, hakuna nchi ya kigeni yenye haki ya kuendesha jela za siri ndani ya Afghanistan na kwamba kushikiliwa raia wa nchi hiyo na wanajeshi wa kigeni kunakinzana na haki ya kujitawala ya nchi hiyo.
Wanajeshi vamizi wa Uingereza wanawashikilia Waafghani hao katika jela ya Bastion katika jimbo la kusini la Helmand kwa muda mrefu bila kuwafungulia mashtaka. Hii ni katika hali ambayo vikosi hivyo vinaruhusiwa kuwashikilia washukiwa kwa siku 4 tu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO