Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa, serikali yake itaendelea na mpango wa ujenzi katika bustani mashuhuri ya Gezi mjini Istanbul licha ya kuendelea maandamano makubwa ya kupinga mipango hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari nchini Tunisia, Erdogan amesema wageni ndio wanaochochea maandamano hayo na kwamba raia kadhaa wa kigeni wamekamatwa. Hii ni katika hali ambayo, afisa mmoja wa polisi amefariki dunia leo Alhamisi baada ya kushambuliwa na waandamanaji wenye hasira mjini Istanbul. Matamshi ya Erdogan yamesababisha mtikisiko mkubwa wa kiuchumi kwani Lira ya Uturuki imepoteza dhamani dhidi ya dola huku hisa za serikali zikipungua thamani punde baada ya kutolewa kauli hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO