Majeshi ya Yemen yameanza leo operesheni kubwa dhidi ya makundi yenye mafungamano na al-Qaeda ambayo hivi karibuni yameteka vijiji kusini mashariki ya jimbo la Hadramawt. Afisa wa jeshi amesema kuwa vikosi vya jeshi la serikali vikisaidiwa na vifaru na helikopta vimeanzisha operesheni alfajiri ya leo katika eneo la Ghayl Bawazir kiasi ya kilometa 30 mashariki ya mji wa bandari wa Mukalla.
Watu walioshuhudia wamesema kuwa wameona milolongo ya magari ya jeshi ikielekea katika eneo hilo, ambalo maafisa wanasema lilikamatwa na watu wenye silaha wa kundi la al-Qaeda mwezi uliopita. Wanajeshi saba na raia watatu wamejeruhiwa na kupelekwa Hospitalini mjini Mukalla. Wapiganaji wa al-Qaeda wamekuwa wakijikusanya upya tangu mwezi Juni 2012 katika maeneo ya Hadramawt baada ya kufurushwa kutoka katika jimbo hilo la kusini la Abyan ambako wanadhibiti miji mikubwa kwa zaidi ya mwaka sasa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO