Waandamanaji wamepambana na polisi nchini Uturuki usiku wa kuamkia leo licha ya serikali kuomba msamaha kutokana na polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji hao. Naibu waziri mkuu wa Uturuki Bulent Arinc ameomba radhi kwa waandamanaji ikiwa ni juhudi za kusitisha wimbi hilo kubwa la maandamano dhidi ya waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan.
Naibu waziri mkuu Bulent Arinc anatarajiwa kukutana leo na watayarishaji wa chanzo cha maandamano dhidi ya mipango ya kujenga jengo litakalokuwa na maduka lililo katika mfano wa banda la enzi za utawala wa himaya ya Ottoman katika bustani maarufu ya mjini Istanbul katika uwanja wa Taksim. Lakini amekataa kuzungumza na baadhi ya makundi ambayo anayashutumu kwa kutumia hali hiyo na kuchochea ghasia.
Wakati huo huo polisi wametumia mabomba ya maji na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokusanyika kwa usiku wa tano mjini Istanbul na Ankara.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO