Friday, June 21, 2013

UN YAKOSOA NJAMA ZA ISRAEL JUU YA WATOTO

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limekuwa likiwatumia watoto wa Kipalestina kama ngao ya kibinadamu. Taarifa iliyotolewa jana na kamati ya haki za watoto ya Umoja wa Mataifa imekosoa vikali vitendo vya majeshi ya Israel vya kuwatesa watoto wa Kipalestina na kusisitiza kuwa, majeshi ya Israel mara nyingi yamekuwa yakiwatumia watoto  hao kama ngao za kibinadamu kwenye oparesheni zao za kijeshi. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, watoto  wa Kipalestina pia wanakosa huduma muhimu za afya, elimu na hata maji salama ya kunywa. Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, watoto wa Kipalestina wanaotiwa mbaroni huteswa na majeshi na polisi ya Israel, na hata wamekuwa wakilazimishwa kukubali makosa, ili waweze kuachiliwa huru. Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, katika kipindi cha miaka 10 ya hivi karibuni, karibu watoto elfu saba wa Kipalestina wenye umri wa kati ya miaka 9 hadi 17 walitiwa mbaroni na majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO