Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameusia:
(( أُوصِيكُمْ بِتَقْوى اللَّه، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وإِنْ تَأَمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حبشيٌ ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيرى اخْتِلافاً كثِيرا . فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وَسُنَّةِ الْخُلُفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ ، عضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ ، وإِيَّاكُمْ ومُحْدثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضلالَةٌ )) رواه أبو داود ، والترمذِي وقال حديث حسن صحيح
((Nakuusieni kumcha Allaah, usikivu na twaa hata ikiwa kiongozi wenu (Au atakayekuamrisheni) ni Mtumwa wa Habash. Mtakaoishi miongoni mwenu mtaona ikhtilafu nyingi. Kwa hiyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa waliongoka baada yangu. Ziumeni kwa magego (zikamateni kwa nguvu wala msiziache). Na tahadharini na mambo ya uzushi kwani kila bid'ah ni upotofu)) [Abu Daawuud, At-Tirmidhiy kasema Hadiyth Hasan Swahiyh]
Na ametahadharisha:
( إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمد صلى الله علي وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار)) أخرجه مسلم في صحيحه
((Maneno bora ni kitabu cha Allah (Qur-aan) na Uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika dini) ni bid'ah (uzushi) na kila bid'ah ni motoni)) [Muslim katika Swahiyh yake]
Ndugu Wapenzi Waislam,
Tunaukaribia mwezi Mtukufu wa Ramadhaan. Mwezi wenye fadhila tele zisizohesabika idadi yake. Mwezi ambao ndani yake utakapofunga Swawm yake kwa Iymaan ya dhati na kuitakidi kuwa kuna malipo, basi utasamehewa madhambi yako yaliyotangulia. Mwezi ambao haufananishwi na miezi mingine kwa mavuno na ujira, du’aa ya mfungaji haikataliwi, anapofunga Muislam huwa na furaha mbili; furaha wakati anapofungua na furaha wakati anapokutana na Mola wake. Mwezi ambao Swawm itamuombea shufaa mja siku ya Qiyaamah, itakaposema siku hiyo kumuambia Allah, “Ee Mola, nimemzuia chakula chake, na matamanio yake ya kimwili mchana kutwa, basi niache nimwombee Shafa'ah.”
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO