Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Bi. Catherine Ashton leo Jumatatu amemtaka Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry kutoa maelezo kuhusu tuhuma zilizotolewa na afisa wa zamani wa CIA kwamba vyombo vya usalama vya nchi yake vimekuwa vikiwafanyia ujasusi wanadiplomasia wa EU.
Duru za habari zinaarifu kwamba, Kerry alipatwa na kigugumizi alipotakiwa kutoa maelezo hayo ambapo amesema hajui lolote kuhusiana na tuhuma hizo. Waziri John Kerry amesema atatoa taarifa kamili baada ya kujua mbivu na mbichi kuhusu kadhia hiyo.
Afisa wa zamani wa CIA, Edward Snowden ameliambia jarida la Der Spiegel la Ujerumani kwamba, Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani (NSA) limekuwa likiwachunguza kwa siri na kuwafanyia ujasusi wanadiplomasia wa EU katika miji ya Washington, New York na Brussels. Jambo hilo limelaaniwa vikali na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO