Ralph Schoenman mchambuzi wa masuala ya kisiasa kimataifa amesema kuwa wimbi la mashambulizi linaloendelea dhidi ya kanali za matangazo za Iran ni kampeni inayotekelezwa na Washington ili kuandaa uwanja wa kuvamiwa kijeshi Iran. Schoenman amesema kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya ubeberu wa Marekani wa kutaka kuanzisha anga ya vita na Iran. Ameongeza kuwa kitendo cha kufungia matangazo ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB ni jaribio lenye lengo la kuwatisha wananchi wa Iran na kuwazuia walimwengu kusikiliza maoni na mitazamo inayotolewa na nchi zote zilizo chini ya mashambulizi na zile zinazolengwa na ubeberu wa Marekani.
Mashirika kadhaa ya huduma za satalaiti duniani yakiwemo ya Eutelsat na Intelsat yamesimamisha kurusha matangazo ya kanali kadhaa za Iran. Intelsat ilisema Juni 19 mwaka huu kuwa haitatoa tena huduma kwa kanali za Iran ikiwemo televisheni ya Press kuanzia leo Julai Mosi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO