Friday, July 12, 2013

LIBYA YASEMA UHUSIANO WAKE NA MISRI UTAENDELEA

Balozi wa Libya mjini Cairo, Misri, amesema kuwa, hatua ya kuwaondosha madarakani Ikhwanul Muslimin nchini Misri, haitoathiri mahusiano ya nchi hizo mbili jirani. Faiz Jibril, amesema, kuwepo madarakani Ikhwanul Muslimin au kutokuwepo kwao, hakutaathiri katu uhusiano kati ya Tripoli na Cairo. Ameongeza kuwa, msingi wa mahusiano ya nchi hizo mbili ni kunadhaminiwa manufaa ya pande mbili. Jibril ameongeza kuwa, kabla ya mapinduzi, taifa la Libya lilikuwa tayari limewekeza nchini Misri kiasi cha dola bilioni 10 hadi 12 kwa minajili ya kuinua kiwango cha uchumi wa Misri. Muhammad Mursi, aliondolewa madarakani tarehe 3 Julai mwaka huu na jeshi la nchi Misri baada ya kushadidi maandamano ya wawapinzani wake. Suala hilo liliibua machafuko baina ya wapinzani na waungaji mkono wa rais huyo aliyeenguliwa madarakani na kulilazimu jeshi hilo kuingilia kati machafuko hayo mara mbili ambapo tarehe 8 mwezi huu liliwafyatulia risasi waandamanaji wanaomuunga mkono rais huyo na kuuwa watu zaidi ya 50.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO