Tuesday, July 02, 2013

NETANYAHU AKATAA KUSISMAMISHA UJENZI

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amekataa masharti ya Wapalestina kwa ajili ya kufanya mazungumzo. Wapalestina wanaitaka Israel isimamishe ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi na iwaachie huru wafungwa wa Kipalestina kama sharti la kufanya mazungumzo na Tel Aviv. Akizungumza hivi karibuni na waziri wa ngazi ya juu wa Israel, Netanyahu alisema kuwa hana nia ya kutangaza kusimamisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan au kuwaachia huru wafungwa wa Kipalestina kama sharti la kuanza mazungumzo kati ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala wa Tel Aviv. Waziri huyo wa ngazi ya juu wa utawala wa Kizayuni amesema Benjamin Netanyahu amekataa masharti hayo ya Wapalestina na kwamba anataka kuanza mazungumzo hayo bila ya masharti yoyote.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO