Ufaransa imeanza kutoa mbinyo kwa Umoja wa Ulaya kuchelewesha mazungumzo na Marekani kuhusu mpango mkubwa wa biashara huru kutokana na madai ya Marekani kufanya ujasusi katika ofisi za Umoja wa Ulaya, lakini Ujerumani imesema mazungumzo hayo yanapaswa kuendelea kama yalivyopangwa. Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ambaye amesema mazungumzo na Marekani hayapaswi kuendelea bila ya hakikisho kuwa upelelezi umesitishwa, alikuwa anatarajiwa kukutana na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, baadaye leo mjini Berlin.
Mkuu wa tovuti inayofichua siri ya Wikileaks wakati huo huo ameyaomba mataifa ya Ulaya kumpatia hifadhi ya kisiasa mfanyakazi wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani, Edward Snowden, ambaye hatua yake ya kuvujisha mtandao mkubwa wa Marekani wa ujasusi dhidi ya washirika wake umezusha wasiwasi mkubwa. Mazungumzo kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya katika kile ambacho kinaelezwa kuwa makubaliano makubwa ya kibiashara ambayo hayajawahi kujadiliwa. Majadiliano hayo yanatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo mjini Washington.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO