Wednesday, October 17, 2012

KUKAMATWA KWA SHEIKH ISSA PONDA.

TAARIFA YA DHARURA 
Asalaam Alaykum! 
Saa 4 asubuhi nilifika Central Police 
kusimamia mahojiano yake na Polisi kwa mujibu wa haki za mtuhumiwa nilionana na msaidizi wa ZCO daada ya utambulisho na kumfahamisha haki zake wakati wa mahojiano alihojiwa. Ukiacha namna alivyokamatwa mpaka naondoka polisi saa 10 kasoro alikuwa ktk hali nzuri na polisi akiwa kituoni
hawakumfanyia lolote lililokinyume na haki za mtu aliyechini ya ulinzi. 
Sheikh anatuhumiwa na mambo yafuatayo:
- 1. Kuhamasisha maandamano kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati wa mahojiano walitaka kujua yafuatayo:-
                  i. kwanini waliandamana
                 ii. nani aliandaa mabango
                iii. kwanini walisema kuwa baada ya maandamano yale wataenda    

                     kumng'oa Mufti na Ndalichako

                iv. nani aliandaa maandamano Sheikh alikiri kuhamasisha 

                    maandamano na pia alikubali ujumbe uliuokuwa katika mabango 

                    ulikuwa umebeba hisia za waislamu. Isipokuwa yeye hajui nani 
                    aliyaandika hayo mabango.

 Kuhusu Mufti na Ndalichako alisema wanastahili kuondolewa kwasababu ya kuongoza kwa dhulma dhidi ya waislamu. Pia alisema maandamano yaliandaliwa na Taasisi na Jumuiya za Kiislamu na yeye ni katibu wake.

 2. Kuvamia kiwanja cha chang'ombe Hapa alijibu kuwa huo ni mgogoro wa ardhi na waislamu wapo pale kwasababu ni kiwanja cha waislamu. Na kama kuna mtu anadai amevamiwa eneo lake huo ni mgogoro wa ardhi
aende kushitaki mahakama ya ardhi na waislamu wapo tayari kufika mahakamani kujibu. Pia alikiri kuwa amehusika ktk ujenzi wa msikiti unaojengwa ktk eneo hilo.

 3. Kuhamasisha maandamano kidongo chekundu 
 
4. Vurugu mbagala. Haya mawili ya mwisho hakuhojiwa kwasababu mafaili yanayohusu malalamiko hayo yalikuwa hayajafika central lakini vilevile muda ulikuwa umeenda sana. Kwani mpaka tunamaliza mahojiano ilikuwa ni saa kumi kasoro hivi toka saa nne asubuhi. DHAMANA. Baada ya mahojiano niliomba apatiwe dhamana na kesho afike polisi kwa mahojiano zaidi. Polisi waliokuwa wanamhoji walikataa kwa hoja kuwa suala hilo liko kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi. Waliomba nikamwone ZCO Bw. Msangi, yeye alisema hawezi kulitolea maamuzi akanitaka nimwone Kamanda Kova. Nilienda kuonana na Kamanda Kova naye aliniambia kuwa hawawezi kutoa dhamana mpaka amalize mahojiano yaliyobaki. Na vile vile alisema wanasubiri wapate ushauri toka ofisi ya DPP. Lakini zaidi akasema kwa kuwa issue ya mbagala kuna watu wameshitakiwa kwa armed robbery kosa ambalo halina dhamana si vizuri kumpa dhamana sasa kwani huenda katika upelelezi wao wanaweza kumuunganisha na washitakiwa wa armed robbery mbagala. Kwa ufupi hiyo ndio hali iliyokuwepo. 


NAOMBA WAISLAMU WAAMBIWE WAWE NA SUBIRA WAKATI HUU WAIFANYE LOLOTE LITAKALOWAPA NAFASI MAADUI WA UISLAMU MANENO YA KUSEMA Maasalamu!
By Brother Juma Nassoro - Wakili





















No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO