SHULE ya Sekondari Kibiti imeifungwa shule kwa madai ya mgogoro wa kidini hivyo 
wanafunzi kupewa saa mbili kutoonekana shuleni hapo vinginevyo watachukuliwa 
hatua za kisheria.
Kufungwa kwa shule hiyo kumefikiwa na Bodi 
iliyokutana  na kuamua kuifunga shule hiyo kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa 
matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na hisia za kidini zinazozidi kukua kwa 
kasi shuleni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu, amethibitisha 
kufungwa kwa shule hiyo.
“Sipo Rufiji lakini nimejulishwa kuhusiana na 
kufungwa kwa shule hiyo,”alisema kwa ufupi.
Chanzo cha kufungwa kwa shule 
hiyo inadaiwa kuwa ni malalamiko ya pande zote mbili baina ya wanafunzi Waislam 
na Wakikristo ambao wamekuwa wakilaumiana kila upande kudhalilisha dini ya 
mwenzake hapo shuleni.
Mmoja wa wanafunzi hao wa dini ya kiislam ambaye 
aliomba asitajwe jina na kudai kuwa waislam wanalalamika kuwa wakiwa wanafanya 
ibada katika eneo hilo wenzao wa dini ya kikristo huwafanyia 
fujo.
Alisema kuwa sababu nyingine ni kwamba wanafunzi wenzao siku moja 
walikwenda kutafuta nyama ya nguruwe na kuja kuitumia katika vyombo 
vinavyotumika shuleni hapo.
Kwa upande wa wanafunzi wa kikristo wao 
wanasema kuwa wanafunzi wenzao walichana chana Biblia na kuchoma ofisi yao ya 
kidini iliyopo hapo  shuleni .
Alisema kuwa bodi ya shule imelazimika 
kuifunga shule hiyo kwa muda usiojulikana ili kuepuka vurugu kutokea shuleni 
hapo ili wapate muda wa kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.
Mmoja wa 
wanafunzi hao alisema kuwa wanafunzi hao walilalamikia suala hilo kwa muda mrefu 
bila kupatiwa ufumbuzi na ndipo kukawa na mgomo wa hapa na pale wakiutuhumu 
uongozi wa shule hiyo kwa kushindwa kuthibiti malalamiko 
hayo.
 Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana Mkuu wa shule hiyo, 
Leslaus Kihongosi alithibitisha kufungwa kwa shule hiyo lakini akasema kuwa 
hawezi kuwa msemaji wa suala hilo kwa kuwa sio mmiliki wa shule 
hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji anayedaiwa 
kuwa mmiliki wa shule hiyo  Nasoro Mwingira alipoulizwa kuhusiana na kufungwa 
kwa shule hiyo alisema kuwa amepata taarifa za tukio hilo.
“Nasema kwa 
sasa siwezi kuzungumza jambo lolote kwa kuwa naelekea kwenye tukio  nipo 
njiani,”alisema.
Diwani wa kata ya Mtawanya iliyopo shule hiyo ya 
kitaifa,  Rashidi Mkinga alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa 
analisikia mitaani na hakushirikishwa katika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo na 
yeye hawezi kusema lolote.
Haijafahamika mgogoro wa kidini baina ya 
wanafunzi wa dini mbili hizo umeanza lini kutokana na wahusika kukwepa 
kulizungumzia suala hilo huku wakitupiana mpira.
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO