Monday, December 03, 2012

CATHERINE ASHTON ATAKA ISRAEL IHESHIMU MAKUBALIANO


Catherine Ashton Mkuu wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa uendelezaji wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unakinzana na sheria za kimataifa na kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ufungamane kikamilifu na ahadi zake za kuanzishwa tena mazungumzo ya amani kati ya Wazayuni na Wapalestina. Bi. Ashton amewataka viongozi wa utawala wa Israel wafute kabisa mpango wa ujenzi wa vitongoji vipya vitakavyokuwa na nyumba elfu tatu za makaazi katika maeneo ya Baitul Muqaddas na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. 


Ameongeza kuwa, mpango huo wa ujenzi wa vitongoji bila shaka utakwamisha juhudi za kuanzishwa tena mazungumzo kati ya Wapalestina na Wazayuni.
Wakati huohuo, baraza la mawaziri la utawala wa Israel limepitisha mpango wa ujenzi wa Sinagogi mkabala wa Masjidul Aqswa. Taarifa zinasema, hatua hiyo imechukuliwa baada ya kupandishwa hadhi ya Palestina hivi karibuni kwenye kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa kuichagua kuwa nchi mtazamaji na wala siyo mwanachama wa umoja huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO