Tuesday, December 04, 2012

HAMAS SI KUNDI LA MAGAIDI ISIHUSHWE NAO


Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Bunge la Iran amesema, kwenda sambamba malengo ya Hamas na Makubaliano ya Umoja wa Mataifa kunalazimu kuiondoa harakati hiyo katika makundi ya kigaidi. Nouzar Shafii ameashiria takwa la Ismail Haniya la kuondolewa harakati hiyo ya  mapambano ya Kiislamu ya Palestina katika orodha ya makundi ya kigaidi na kuongeza kuwa, Wamarekani wameiweka harakati hiyo kwenye orodha ya magaidi kutokana na sababu za kisiasa na kuunga mkono kibubusa utawala wa Kizayuni wa Israel.  Mbunge huyo wa Iran aidha amesema kwamba falsafa ya kuundwa Hamas ni kupigania ukombozi na huru, malengo ambayo ndio sura halisi ya makubaliano ya Umoja wa Mataifa na kwa ajili hiyo basi Hamas inapaswa kundolewa katika makundi ya kigaidi. 
 Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Bunge la Iran pia  amekumbusha mashambulizi ya siku 8 ya Wazayuni dhidi ya Gaza na kusema kwamba, harakati ya Hamas lililazimika kutumia silaha baada ya kuzingirwa kikamilifu na Israel na haipaswi kuwekwa katika orodha ya magaidi na makundi kama al Qaida na Taliban.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO