Thursday, December 13, 2012

MAREKANI IMEANZISHA VITA DHIDI YA WAISLAM

Imam wa Masjidul Islam mjini Washington nchini Marekani amesema kuwa, Marekani imeanzisha vita vya pande zote dhidi ya Uislamu na Waislamu. Sheikh AbdulA'lim Mussa amesema kuwa, vita vilivyoanzishwa na Marekani na waitifaki wake kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, kwa hakika ni vita dhidi ya Uislamu na Waislamu na si katika eneo la Mashariki ya Kati pekee, bali katika ulimwengu mzima. Sheikh AbdulA'lim Mussa ameongeza kuwa, hivi sasa Marekani na Uingereza zimepoteza nguvu zao ulimwenguni na wala hazina uwezo wa kutekeleza jambo lolote chanya ulimwenguni. Imamu wa Masjidul Islam mjini Washington ameongeza kuwa, wakati umefika kwa Waislamu kuzindukana na kufanya juhudi na idili ya kukabiliana na njama hizo chafu za nchi za Magharibi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO