Saturday, December 01, 2012

MPALESTINA MMOJA AULIWA HUKO GHAZA

Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiuka makubaliano ya kusitisha vita huko Ghaza na kumuuwa shahidi kijana mmoja wa Kipalestina mkazi wa eneo hilo. Duru za hospitali za Palestina zimearifu kuwa Mahmoud Jarhun aliyekuwa na miaka 21 ameuliwa shahidi kwa kufyatuliwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni huko mashariki mwa mji wa Rafah. Hii ni katika hali ambayo Wapalestina wangine 11  walijeruhiwa jana kwa risasi na wanajeshi wa Israel  huko katika eneo kati ya mpaka wa Ukanda wa Ghaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Mashambulizi ya siku nane ya jeshi la Israel huko Ghaza yalianza siku ya Jumatano  ya tarehe 14 Novemba na kuendelea hadi Jumatano  Novemba 21 hata hivyo utawala huo ghasibu mwishowe ulilazimika kukubali kusimamisha vita ulivyovianzisha dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza kutokana na muqawama mkubwa ulioonyeshwa na Wapalestina.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO