Thursday, December 13, 2012

NOUR AL-MALIK: HATUTAKI MAREKANI KUWA MPATANISHI WETU

Waziri Mkuu wa Iraq Nour al Maliki, amekataa ombi la baadhi ya nchi ikiwemo Marekani kuwa mpatanishi kati ya serikali ya Baghdad na mji wa Arbil nchini humo. Duru za habari kutoka Iraq leo zimearifu kuwa, katika siku za hivi karibuni Waziri Mkuu huyo wa Iraq, alipokea maombi kutoka kwa nchi kadhaa ikiwemo serikali ya Washington zikitaka kuwa mpatanishi katika mgogoro uliopo kati ya serikali ya Baghdad na Arbil lakini al Maliki amekataa ombi hilo na kuongeza kuwa, mgogoro uliopo kati ya pande mbili, ni mgogoro wa ndani usiofaa kuingiliwa na madola ya nje ikiwemo Marekani. Duru hizo zimeongeza kuwa, Waziri Mkuu wa Iraq Nour al Maliki amezitaka nchi hizo kutoingilia masuala ya ndani ya Iraq na kwamba, Iraq yenyewe inao uwezo wa kujitatulia mambo yake. 


Tofauti kati ya Baghdad na Arbil zilizuka baada ya amri ya waziri mkuu huyo ya kutaka kuundwa kikosi maalum kitakachosimamiwa na vikosi vya Dujail kwa ajili ya kuimarisha usalama katika miji ya Kirkuk, Diyala na Salah ad Din, tofauti ambazo zimepelekea kuzuka mapigano kati ya vikosi vya serikali na vile vya eneo la Tuz Khormato katika eneo la Kurdistan nchini humo.
Sujafa habari usiku 13/12/2012

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO