Thursday, December 06, 2012

TETEMEKO LA ARDHI IRAN


Watu wasiopungua 8 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa, katika mtetemeko wa ardhi uliokuwa na ukubwa wa 5.5 kwa kipimo cha Rishta uliotokea mashariki mwa Iran. Zilzala hiyo ilitokea usiku wa kuamkia leo katika mkoa wa Khorasani Kusini na taarifa zinasema kuwa, imeharibu majengo na kukata nyaya za umeme na mawasiliano ya simu. 


Iran ni miongoni mwa maeneo yanayokumbwa na mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara ambapo mwezi wa Agosti mwaka huu watu zaidi ya 300 walifariki dunia na wengine zaidi ya 3,000 kujeruhiwa katika mtetemeko mkubwa uliokumba eneo la kaskazini mashariki mwa nchi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO