Tuesday, January 01, 2013

HILLARY CLINTON DAMU YAGANDA KWENYE UBONGO

Hillary Clinton Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani amelazwa kwenye hospitali moja mjini New York, baada ya kugunduliwa tatizo la kuganda damu kwenye ubongo wake. Kumekuwa na uvumi mwingi kuhusiana na hali yake ya kiafya baada ya kupoteza fahamu na kuanguka siku chache zilizopita, lakini madaktari wamebaini kwamba kuna damu iliyoganda kwenye ubongo wa Clinton. Timu ya madaktari imeeleza kuwa bado zinafanyika juhudi za kumpa madawa ili kuondoa damu hiyo kwenye ubongo. Hillary Clinton mwenye umri wa miaka 65 alikimbizwa hospitali baada ya  kudhoofika hali yake ya kimwili pamoja na kukabiliwa na  tatizo la kutofanya vyema mmeng'enyeko wa chakula kwenye mwili wake. Madaktari wanasema kuwa, tatizo la mgando wa damu kwenye ubongo ni la  hatari mno kwani linaweza kusababisha mgonjwa kupooza mwili au kufariki dunia.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO