Tuesday, January 08, 2013

M15 INAWALAZIMISHA WASOMALI KUFANYA UJASUSI


Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza khususan shirika la ujasusi la MI 5 yanatuhumiwa kuwashinikiza Wasomali Waingereza kuyafanyia ujasusi katika jamii yao huko Uingereza. Wasomali Waingereza wapatao laki nne wameeleza kukasirishwa sana na namna wanavyofanyiwa wakiwa katika mipaka ya Uingereza ambapo wengi wao wamelalamika namna shirika la ujasusi la nchi hiyo MI 5 linavyowalazimisha kuwafanyia ujasusi wenzao wenye asili ya Kisomali. Hayo yameripotiwa na gazeti la Independent.
Mohammed Elmi kiongozi wa raia wa Somalia wanaoishi nchini Uingereza amesema kuwa  Wakuu wa  Kisomali  huko London walifanya mkutano wao kabla ya sikukuu ya Krismasi ili kujadili suala hillo. Amesema jamii ya Kisomali iko tayari kushirikiana na serikali ya Uingereza kuhusu masuala ya usalama na kwamba kile kisichokubalika ni aina yoyote ya kushurutishwa au kushinikwa jamii yao. Gazeti la Independent lilifichua kwa mara ya kwanza juu ya mbinu zilizotumiwa na mashirika ya kijasusi ya Uingereza  mwaka 2009 pale lilipoandika katika ripoti yake kwamba idara za usalama za Uingereza zilitishia kuwawekea vikwazo wanaume watano Waislamu wa Afrika Mashariki  iwapo hawangekubali kushirikiana na idara hizo za ujasusi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO