Tuesday, January 08, 2013

NORWAY YAPIGA MARUFUKU ASKARI WA KIKE KUVAA HIJAB


Maafisa wa polisi wanawake wa Kiislamu nchini Norway wamepigwa marufuku kuvaa hijabu ya Kiislamu wakiwa kazini.
Waziri wa Utamaduni wa Norway amepinga pendekezo la kamati iliyoundwa nchini humo na kusisitiza kuwa, maafisa wa polisi wa kike hawatakuwa na ruhusa ya kuvaa hijabu ya Kiislamu kama sehemu ya sare zao za jeshi.
Hivi karibuni serikali ya Norway iliunda jopo la watu 15 ambalo lilitoa pendekezo la kuruhusiwa askari wa kike wa Kiislamu kuvaa vitambaa vya kichwa ikiwa ni sehemu ya sare zao. Taarifa zinasema kuwa, vyama vingi vya kisiasa nchini Norway vimetangaza upinzani wao juu ya kubadilishwa sheria za mavazi ya polisi wa kike nchini humo ili kutoa fursa ya kutumiwa mavazi yanayoendana na sheria za kidini.Sakata la hijabu nchini Norway lilianza mwaka 2008 wakati mwanamke mmoja wa Kiislamu alipotaka kuvaa hijabu wakati akiwa kwenye mafunzo ya jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO