Tuesday, January 01, 2013

MASHIA WAZIDI KUULIWA PAKISTAN

Hapo juzi Jumapili idadi ya watu 19 waliuawa na wengine 25 kujeruhiwa, katika shambulio la kigaidi, lililolilenga basi la wafanya ziara wa Kishia katika mkoa wa Baluchistan nchini Pakistan. Shambulio hilo lilitokea baada ya mabasi matatu yaliyokuwa yamewabeba Waislamu wa Kishia wa Pakistan, waliokuwa wakielekea Iran, kulipuliwa kwa mabomu yaliyokuwa yametegwa katika gari katika wilaya ya Mastung, yapata kilomita 35 kusini mwa mji wa Quetta katika mkoa huo wa Baluchistan. Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari amelaani mashambulizi hayo na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za mashahidi wa tukio hilo. 

Wislamu hao walikuwa wakielekea katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kuruzu haram tukufu ya Imam Ridha (as) na maeneo mengine matakatifu nchini hapa. Wimbi la mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Waislamu katika maeneo tofauti ya Pakistan, limeshuhudiwa katika mwaka huu wa 2012 unaomalizika hii leo, mashambulizi ambayo yamepelekea kuuawa kwa mamia ya watu na kuwajeruhiwa wengine wengi. Mashambulizi dhidi ya Waislamu katika misikiti, husseiniya za maombolezo ya ya kifo cha Imam Hussein (as) na wasomi mbalimbali wa Kishia na Kisuni ni miongoni mwa vitendo vya kigaidi vinavyotekelezwa na magaidi wenye mielekeo ya kimadhehebu nchini Pakistan. Jinai hizo bila shaka zinafanyika kwa lengo la kuzusha fitina na vita vya ndani nchini humo. Daima wapiganaji wa makundi ya Jahanguye na jeshi Sahaba wamekuwa wakitangaza kuhusika na mashambulizi hayo ya kigaidi dhidi ya Waislamu wa Pakistan na hivi karibuni kundi jingine linalofahamika kwa jila la Tahrik Twaliban liliungana na makundi hayo na hivyo kushadidisha zaidi vitendo hivyo vya kigaidi. Duru nyingi za kisiasa na kimadhehebu nchini humo zinaamini kuwa, makundi hayo ya kigaidi yenye mielekeo ya kimadhehebu yanayopata uungaji mkono wa kifedha kutoka kwa mataifa ya kigeni, yameathiriwa na kufuata mafundisho yasiyo sahihi katika kutekeleza jinai hizo. Kwa maana nyingine ni kwamba, duru za nje, hazitaki kuona hali ya amani na uthabiti vikitanda nchini Pakistan hivyo mauaji na mashambulizi ya kigaidi yanakusudia kuzusha vita vya ndani nchini humo. Kwa kauli nyingine ni kwamba, viongozi wa Kishia na Kisuni nchini Pakistan wanachochewa kuvunja umoja na mshikamano wao na kuanza kupigana wao kwa wao. Katika hali hiyo, ni wazi kuwa viongozi, maafisa wa usalama na wanazuoni wa Pakistan wanakabiliwa na majukumu mazito ya kurejesha amani na usalama nchini humo kwa kukabiliana na njama za maadui wa taifa hilo

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO