Upinzani nchini Venezuela umesema kuwa unakwenda mahakamani kuitaka mahakama kuu kuamua iwapo katiba ya nchi hiyo inaruhusu kucheleweshwa kwa sherehe za kuapishwa rais Hugo Chavez ambaye anaugua ugonjwa wa saratani. Tangazo hilo la kiongozi wa upinzani Ramon Guillermo Aveledo limekuja baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura kuahirisha sherehe za kuapishwa kwa Chavez, ambako kumepangwa kufanyika kesho Alhamis. Makamu wa rais Nicolas Maduro amesema kuwa ataiongoza nchi hiyo hadi pale rais Chavez atakaporejea.
Aveledo hakusema ni lini ama ni vipi upinzani unaazimia kuyafikisha madai yake hayo mahakamani. Rais wa mahakama kuu Luisa Estella Morales anatarajiwa kuwa na mkutano na vyombo vya habari leo na anaweza kuzungumzia jukumu la mahakama katika mzozo huo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO