Friday, March 22, 2013

NTAGANDA YUKO NJIANI KUELEKEA THE HAGUE

Mbabe wa kivita wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean Bosco Ntaganda ameondoka nchini Rwanda leo, akiwa chini ya uangalizi wa maafisa wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, kwenda kushtakiwa mjini The Hague. Waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa Ntanganda ameondoka mjini Kigali. ICC pia ilithibitisha kuondoka kwake na kusema katika taarifa kuwa hii ndiyo mara ya kwanza kwa mtuhumiwa kujisalimisha kwa hiari yake mbele ya mahakama hiyo, na kuzishukuru Marekani na Rwanda kwa msaada wao. Ntaganda anakabiliwa na mashtaka saba yanayohusiana na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu aliyoyatenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO