Tuesday, January 08, 2013

WAISLAM WASHAMBULIWA MSIKITINI

Watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya kundi la watu waliokuwa na silaha nchini Nigeria kuwashambulia waumini wa dini ya Kiislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya sala.
Shambulio hilo lilifanyika jana dhidi ya watu waliokuwa wakisali sala ya Alasiri katika mji wa Kano ulioko kaskazini mwa Nigeria. Viongozi wa Nigeria wamesema kuwa, shambulio hilo lilifanywa na watu waliokuwa wamepanda pikipiki. Taarifa ya Polisi inawatuhumu wafuasi wa kundi la Boko Haram kuwa ndio waliotekeleza shambulio hilo. Tokea mwaka 2009 hadi sasa maelfu ya wananchi wa Nigeria wameuawa na wengine kujeruhiwa kutokana na mashambulio yanayofanywa na kundi la Boko Haram

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO