Wabunge kadhaa nchini Uhispania wameikosoa vikali serikali ya nchi hiyo kwa 
kupiga marufuku matangazo ya kanali za Televisheni za Press TV na Hispan TV 
kutokana na mashinikizo ya lobi za Kizayuni na Marekani. Katika barua yao, 
wabunge wa chama cha United Left wameitaka serikali ya Uhispania kutoa maelezo 
iwapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania Jose Manuel Garcia-Margallo alijadili 
suala la kupiga marufuku kanali za Iran wakati alipokutana na lobi za Kizayuni 
Oktoba mwaka 2012. Wabunge hao wamesema mmiliki wa shirika la satalaiti ya 
Eutelsat ana uraia wa Israel na kwamba amekuwa akiongoza njama dhidi ya vyombo 
vya habari vya Iran barani Ulaya. 
Televisheni ya Iran ya Hispan TV hurusha 
matangazo kwa lugha ya Kihispania kwa masaa 24 nayo Press TV hurusha matangazo 
yake kwa lugha ya Kiingereza. Hivi karibuni televisheni za kimataifa za Iran 
Hispan TV pamoja na Press TV zilipigwa marufuku kurusha matangazo yao kupitia 
satalaiti za Ulaya za Eutelsat na Hotbird. Aidha Shirika la Intelsat  limepiga 
marufuku matangazo ya radio na televisheni kadhaa za kimataifa za Iran kufuatia 
mashinikizo ya Umoja wa Ulaya.  Maamuzi hayo ya kupiga marufu vyombo vya habari 
vya Iran ni ishara ya wazi ya undumakuwili wa nchi za Magharibi zinazodai 
kutetea uhuru wa maoni. Nchi za Ulaya na Marekani zikishirikiana na utawala wa 
Kizayuni wa Israel zinajaribu kuzima sauti ya haki ya vyombo vya habari vya 
Iran.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO