Korea Kaskazini imetishia kuishambulia Korea  Kusini, kama utawala mjini Seoul utaunga mkono  vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi  hiyo. Onyo hilo la Korea Kaskazini limetolewa wakati  ambapo Marekani imetangaza vikwazo zaidi vya  kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini, kufuatia hatua ya  nchi hiyo kutuma roketi ya setilaiti angani mwezi  uliyopita. Korea Kaskazini imemuonya jirani wa  kusini kuwa vikwazo vinamanisha kutangaza vita  dhidi yao. Korea Kaskazini ilitangaza wiki hii kususia  mazungumzo yote yanayolenga kusitisha mpango  wake wa nyuklia, na kuapa kufanya majaribio zaidi  ya roketi na nyuklia, baada ya Baraza la Usalama la  Umoja wa Mataifa kuituhumu kwa jaribio la kombora  la masafa marefu Desemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO